?>

Umoja wa Afrika waanza upatanishi katika mzozo wa Sudan na Ethiopia

Umoja wa Afrika waanza upatanishi katika mzozo wa Sudan na Ethiopia

Duru za kuaminika nchini Sudan zimeripoti kuwa, mjumbe wa Umoja wa Afrika alitazamiwa kuwasili Khartoum akiongoza ujumbe wa upatanishi wa umoja huo katika mzozo wa mpakani baina ya Sudan na Ethiopia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mohamed El Hassan Ould Labat alitazamiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok na Mkuu wa Baraza la Utawala nchini humo, Abdel Fattah al-Burhan kwa ajili ya kupunguza mzozo ulioibuka baina ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Ould Labad mjini Khartoum inafanyika baada ya Sudan kumwita balozi wake nchini Ethiopia Jumatano ya jana kwa mashauriano, kutokana na kuongezeka mzozo wa mpaka baina ya pande hizo mbili ambao umepelekea kutumwa majeshi ya nchi mbili karibu na maeneo ya mpakani katika wiki za hivi karibuni.

Jumapili iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilisema kwamba vikosi vya jeshi la Ethiopia vimevuka mpaka na kuingia Sudan, ikionya kuhusu "athari mbaya" za suala hjilo kwa usalama na utulivu wa eneo hilo.

Mzozo wa mpaka kati ya nchi hizo mbili umeongezeka katika miezi ya hivi karibuni baada ya Sudan kupeleka vikosi vya jeshi kwenye ardhi ambayo ilisema ilikaliwa kwa mabavu na wakulima wa Ethiopia na wanamgambo wa nchi hiyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni