?>

Umoja wa Afrika wakarabisha hatua ya kubatilishwa uamuzi wa kumuongezea muda wa uongozi Rais wa Somalia

Umoja wa Afrika wakarabisha hatua ya kubatilishwa uamuzi wa kumuongezea muda wa uongozi Rais wa Somalia

Umoja wa Afrika umepongeza hatua ya Bunge la Somalia ya kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kumuongezea muda wa uongozi kwa miaka miwili Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmaajo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hayo yamo katika taarifa iliyotolewa na Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ambaye amesisitiza kuwa, umoja hyuo umepongeza na kupokea kwa mikono miwili hatua ya kuachana na uamuzi wa kumuongezea muda wa uongozi kwa miaka miwili Rais wa somalia.

Aidha Umoja wa Afrika umesifu hatua ya Rais wa Somalia ya kutanguliza mbele maslahi ya taifa hilo pamoja na takwa lake la kufanyikka uchaguzi.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, muda si mrefu Umoja wa Afrika utaanisha mwakilishi kwa ajili ya mchakato wa kisiasa nchini Somalia, kama ambayo imetoa wito wa pande na mirengo yote kukaa katika meza moja ya mazungumzo kwa ajili ya kuzitafutia ufuumbuzi hitilafu zilizopo.

Juzi Wabunge wa Somalia walipiga kura na kupasisha uamuzi wa kubatilisha hatua ya awali ya kuongezewa muda wa kubakia madarakani Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kwa muda wa miaka miwili mingine.

IUkumbukwe kuwa, Jumatano iliyopita Rais Mohammad Abdullahi Mohammed wa Somalia alitangaza kuwa, hataongeza muhula wake madarakani kwa muda wa miaka miwili katika kile kilichoonekana kuwa ni kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya kitaifa na kimataifa.

Muhula wake ulimalizika Februari lakini bunge la nchi hiyo hivi karibuni lilimpa idhini ya kutawala kwa miaka mingine miwili, baada ya kukosekana mwafaka wa kufanyika uchaguzi. Hata hivyo baraza la seneti lilipinga uamuzi huo na hivyo kuibua mgogoro mkubwa wa kisiasa

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*