?>

Umoja wa Mataifa: Kunahitajika dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kuwasaidia Wayamen

Umoja wa Mataifa: Kunahitajika dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kuwasaidia Wayamen

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika uratibu wa masuala ya kibinadamu (OCHA) ametangaza kuwa, kunahitajika dola bilioni 3.9 kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya wananchi wa Yemn wanaohitahia misaada ya kibinadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ramesh Rajasingham amesema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, shughuli ya kuwasaidia Wayamen milioni 16 wanaohitajia misaaada ya kibinadamu kwa sasa inakabiliwa na kizingiti kikubwa ambacho ni vyanzo vya fedha kwa ajili ya misaada hiyo.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni vyanzo vya fedha vimepungua mno kiasi kwamba, ni asilimia 58 tu ya fedha zilizokuwa zikihitajia mwaka jana wa 2021 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu ndizo zilizopatikana.

Mwezi uliopita wa Disemba, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ulitangaza kusimamisha misaada kwa raia milioni nane wa Yemen iliyokuwa ikiwahudumia kutokana na nakisi ya bajeti.

Katika miaka 6 ya karibuni Yemen imeathirika na tatizo la uhaba mkubwa wa mafuta, chakula na suhula za kitiba kutokana na kuzingirwa nchi hiyo kwa pande zote na muungano vamizi unaaongozwa na Saudia. 

Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa zilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen Machi 2015 na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa baharini, anga, na nchi kavu. Vita hivyo aidha hadi sasa vimeuwa makumi ya maelfu ya wananchi wa Yemen na kuwafanya mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. 342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*