?>

Umoja wa Mataifa walaani mauaji dhidi ya waandamanaji nchini Myanmar

Umoja wa Mataifa walaani mauaji dhidi ya waandamanaji nchini Myanmar

Umoja wa Mataifa umelaani vikali vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji dhidi ya waandamanaji nchini Myanmar.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vitendo vya ukandamizaji na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya usalama nchini Myanmar dhidi ya waandamanaji wanaolalamikia hatua ya jeshi ya kutwaa madaraka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kutumia vikosi vya mauaji, kuwatisha watu na kuwafanyia maudhi na ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani ni jambo lisilo kubadilika hata kidogo.

Antonio Guterres ametaka kuheshimiwa matokeo ya uchaguzi wa Bunge na kukabidhiwa madaraka ya nchi huko Myanmar kwa utawala wa kiraia.

Hivi majuzi msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric alinukuliwa akisema kuwa, kuendelea kukamatwa wanasiasa, viongozi wa serikali, wanaharakati wa jumuiya za kiraia, wadau wa vyombo vya habari na vilevile kubanwa huduma za intaneti na huduma nyinginezo nchini Myanmar ni mambo yanayotia wasiwasi.

Itakumbukwa kuwa, tarehe Mosi ya mwezi huu wa Februari jeshi la Myanmar lilitangaza kudhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini Myanmar, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi. 

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni