?>

Umoja wa Mataifa walikosoa jeshi Myanmar kwa kundamiza demokrasia

Umoja wa Mataifa walikosoa jeshi Myanmar kwa kundamiza demokrasia

Umoja wa Mataifa umekosoa vikali uamuzi wa utawala wa kijeshi nchini Myanmar wa kuchelewesha uchaguzi na kurefusha hali ya dharura ukisema kuuwa, hatua hiyo inakinzana na matakwa ya kimataifa ya kutaka nchi hiyo irejeshwe katika mkondo wa demokrasia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa amesema hayo baada ya mtawala wa kijeshi wa Myanmar Min Aung Hlaing kujitangaza kuwa Waziri Mkuu siku ya Jumapili na kusema kwamba, ataiongoza nchi wakati wa kipindi cha utawala wa hali ya dharura kilichorefushwa hadi uchaguzi utakapofanyika katika kipindi cha takriban miaka miwil ijayo.

Dujarric amesema, uamuzi huo ni kinyume kabisa na matakwa ya jamii ya kimataifa inayosisitiza udharura wa kurejeshwa nchini Myanmar utawala wa kidemokrasia, wafungwa wote wa kisiasa kuachiliwa huru, machafuko kusitishwa na kukomeshwa ukandamizaji.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza jipya la Utawala la Taifa nchini Myanmar Min Aung Hlaing Jumapili alijitangaza kuwa Waziri Mkuu katika serikali mpya ya mpito na kuahidi kuandaa uchaguzi mpya ifikapo mwaka 2023

Jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi Februari Mosi mwaka huu baada ya kumkamata Rais wa nchi, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo.

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai yake ya kutokea wizi na udanganyifu katika uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana ambapo chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*