?>

Umoja wa Mataifa wasisitiza kuanza uchunguzi kuhusu kuuliwa shahidi mwandishi habari wa al Jazeera

Umoja wa Mataifa wasisitiza kuanza uchunguzi kuhusu kuuliwa shahidi mwandishi habari wa al Jazeera

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametaka kufanyika uchunguzi kamili kuhusu mauaji ya Shireen Abu Akleh mwandishi habari Mpalestina wa televisheni ya al Jazeera yaliyotekelezwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni jana asubuhi walishambulia mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kumuua shahidi mwandishi habari Shireen Abu Akleh aliyekuwa akiiripotia televisheni ya al Jazeera yenye makao yake mjini Doha, Qatar huku akiwa amevalia kizibao chenye nembo ya mwandishi wa habari.  

Farhan Haq Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa jana alisisitiza mbele ya mkutano wa waandishi wa habari kuwa: "Tunataka kufanyika uchunguzi kamil kuhusu mauaji ya mwandishi huyo wa habari na tutasubiri natija ya uchunguzi huo." 

Michel Bachelet Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa pia ameandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba: "Tumeogopeshwa na kushtushwa na kuuawa ripota Shireen Abu Akleh wakati akiripoti kuhusu mashambulizi ya wanajesh wa Israel huko Jenin." 

Afisa huyu wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa: Tunataka kufanyika uchunguzi huru na wa wazi kuhusu mauaji hayo na utoaji kinga ya kutoadhibiwa inapasa kukomeshwa.' 

Wizara ya Afya ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina aidha imetangaza taarifa ya kuuliwa shahidi Shireen Abu Akleh na kueleza kuwa, ripota huyo ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakati akiripoti uvamizi wa Wazayuni dhidi ya kambi ya wakimbizi huko Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Ali al Samudi mfanyakazi mwenzake shahidi Shireen Abu Akleh pia alijeruhiwa katika hujuma ya jana ya Wazayuni; lakini hali yake inaendelea kuboreka.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*