?>

Umoja wa Mataifa wawataka wanajeshi Mali watangaze tarehe ya uchaguzi

Umoja wa Mataifa wawataka wanajeshi Mali watangaze tarehe ya uchaguzi

Umoja wa Mataifa umewataka wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali watangaze tarehe na ratiba ya uchaguzi huku hasira zikiongezeka kutokana na wanajeshi hao kung'ang'ania madaraka wakisema kipindi cha mpito kitachukua miaka mitano kumalizika.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewaambia waandishi wa habari kwamba, ni jambo lisilo na shaka hata kidogo kuwa serikali ya hivi sasa ya Mali ina wajibu wa kutangaza ratiba na tarehe inayokubalika ya uchaguzi. Vile vile amesema ana matumaini atafanya mazungumzo karibuni hivi na mkuu wa mapinduzi ya kijeshi huko Mali.

Aidha amesema, ninashirikiana na ECOWAS na Umoja wa Afrika AU kuandaa mazingira ambayo yataifanya serikali ya Mali ichukue msimamo unaokubalika wa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa raia na juhudi hizo zimekuwa zikifanyika kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na ukaidi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi huko Mali, Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS imelazimika kuongeza mashinikizo yake kwa nchi hiyo maskini ya eneo la Sahel ikiwa ni pamoja na kuifungia mipaka na kuiwekea vikwazo vya kibiashara.

Hatua hizo kali zimechukuliwa baada ya serikali ya mpito ya Mali kupendekeza kubakia madarakani kwa muda wa miaka mitano na kupinga matakwa ya jamii ya kimataifa ya kuheshimu ahadi zake za kuitisha uchaguzi tarehe 27 mwezi ujao wa Februari na kukabidhi madaraka kwa serikali ya raia haraka iwezekanavyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*