?>

Umoja wa Ulaya: Kashfa ya ujasusi unaofanywa na Israel haikubaliki kabisa

Umoja wa Ulaya: Kashfa ya ujasusi unaofanywa na Israel haikubaliki kabisa

Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya amesema kuwa, kashfa ya hivi karibuni ya ujasusi uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel inakinzana na sheria zote za Umoja wa Ulaya.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Bi Ursula von der Leyen alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa, programu ya kijasusi ya Israel iitwayo Pegasus iliyotengenezwa na shirika la Kizayuni la NSO kwa ajili ya kufanya ujasusi katika simu za mkononi za mamia ya waandishi wa habari, wanaharakati wa kisiasa, kijamii na wanasiasa wa kona mbalimbali za dunia, ni jambo ambalo halikubaliki kabisa.

Uchunguzi uliofanywa kwa pamoja na mashirika ya habari ya Reuters, Washington Post, Wall Street Journal, al Jazeera na The Guardian unaonesha kuwa, shirika la kijasusi la NSO la Israel limetumia programu hiyo kufanya ujasusi mkubwa kote ulimwenguni.

Gazeti la New York Times limeandika kuwa, mwaka 2016 ilidaiwa kwamba, prorgamu ya kijasusi ya Pegasus ya Israel ilikuwa inatumiwa dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na waandishi wa habari wa Mexico tu..

Tangu wakati huo gazeti hilo la New York Times lilifichua kuwa, programu hiyo imetengenezwa na Israel ili kuwafanyia ujasusi waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu na wanaharakati wa kisiasa wa Mexico na Saudi Arabia.

Sasa hivi lakini na kwa mujibu wa gazeti hilo kumetolewa ripoti mpya Jumapili wiki hii ambazo zinaonesha kuwa, programu hiyo ya kijasusi ya Israel inatumika kufanya ujasusi dhidi ya nchi nyingi zaidi na dhidi ya watu wengi zaidi duniani.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*