?>

UN: Mzingiro wa Israel dhidi ya watu wa Gaza unakiuka sheria za kimataifa

UN: Mzingiro wa Israel dhidi ya watu wa Gaza unakiuka sheria za kimataifa

Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa huko Palestina amesema kuwa nzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unakiuka sheria za kimataifa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Michael Lynk amesema kuwa, nchi za Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya pia zimekiuka sheria za kimataifa kwa kuipa Israel silaha zinazotumika kushambulia watu wa Gaza na Syria. 

Lynk amesema kuwa, vita na mashambulizi ya mwezi Mei yaliyofanywa na Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yamesababisha hasara ya dola nusu bilioni na kwamba eneo hilo la Palestina linapata maji safi masaa 14 tu kwa siku. Ripota huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kukarabatiwa uharibifu ulisababishwa na mabomu ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza. 

Kuhusu mashambulizi ya karibuni ya Wazayuni huko Palestina, Michael Lynk amesema Baraza la Usalama, Baraza Kuu na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa zimekuwa zikisisitiza kuwa Israel inaendelea kukika haki za binadamu. Amesema azimio nambari 1998 pia linasisitiza kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina ni sawa na kukanyaga na kukiuka haki za binadamu.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*