?>

UN: Vyombo huru vya habari ni msingi wa jamii za kidemokrasia

UN: Vyombo huru vya habari ni msingi wa jamii za kidemokrasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezihimiza serikali "kufanya kila kila lililo ndani ya uwezo wao kusaidia uhuru wa vyombo vya habari, ambao Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaja kama msingi wa jamii za kidemokrasia".

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Antonio Guterres ametoa mwito huo katika ujumbe wake maalum wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Mei, akisisitiza umuhimu wa habari za kuaminika, zilizothibitishwa na zinazoweza kupatikana. 

Katika ujumbe wake huo, Katibu Mkuu wa UN Guterres amebainisha pia hatari binafsi ambazo waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari wanakabiliwa nazo, pamoja na vizuizi, udhibiti, unyanyasaji, mateso, kuwekwa kizuizini na hata kifo, "kwa kufanya tu kazi zao na kwamba hali inaendelea kuwa mbaya.” 

Kwa upande wake, Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, ameangazia umuhimu wa vyombo huru vya habari, visivyochunguzwa na huru, kama "msingi wa jamii za kidemokrasia", vikiwasilisha habari inayookoa maisha, kuboresha ushiriki wa umma, na kuimarisha uwajibikaji na heshima kwa haki za binadamu. 

"Ulimwenguni kote, watu wamezidi kuandamana barabarani kudai haki zao za kiuchumi na kijamii, na pia kukomesha ubaguzi wa kimfumo, kutokujali, na ufisadi", amesema bi Bachelet. 

 Kamishna Mkuu huyo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, ameongeza kuwa, pamoja na hayo, waandishi wa habari wanaotimiza jukumu lao la kimsingi la kuripoti juu ya maandamano hayo ya kijamii wamekuwa walengwa, na wengi wanakuwa wahanga wa matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima na yasiyo na kipimo, kukamatwa kiholela, na kufunguliwa mashtaka ya jinai.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*