?>

UN: Waliohusika na mauaji ya mateka 10 wa kivita Yemen wafunguliwe mashtaka

UN: Waliohusika na mauaji ya mateka 10 wa kivita Yemen wafunguliwe mashtaka

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa akilaani mauaji yaliyofanywa na mamluki na vibaraka wa Saudi Arabia dhidi ya matekani 10 wa vita wa jeshi la Yemen na kusema kuwa mauaji hayo yanakiuka sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Stéphane Dujarric amesema kuwa, mauaji ya mateka wa vita ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na haki za binadamu na kwamba tukio hilo linapaswa kuchunguzwa haraka na wahusika wafikishwe kwenye mkono wa uadilifu. 

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zote kuheshimu sheria za kimataifa na haki za binadamu katika mazingira na hali zote. 

Muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia huko Yemen siku za karibuni uliwanyonga mateka 10 wa kivita wa jeshi la Yemen. Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imesema kuwa hatua hiyo ni jinai ya kivita.

Kamati ya Kitaifa ya Masuala ya Mateka katika Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen inasema: “Uhalifu na jinai hii dhidi ya mateka wa vita wa Yemen ni ushahidi na kielelezo cha sera za nchi vamizi na mamluki wao kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa watu wote wanaokabiliana na uvamizi na vitendo vyao vya kigaidi.”

Utawala wa Saudi Arabia na mamluki wake wameenda mbali zaidi kwa kuwaua mateka wa vita wa Yemen, kuwakata vipandevipande na kutupa maiti zao baharini. 

Wadadisi wa mambo wanasema, kitendo cha kuwaua mateka wa kivita wa Yemen na kutupa maiti zao baharini kinaonesha mporomoko mkubwa wa kimaadili na kutokuwa na dini kwa viongozi wa utawala wa Saudi Arabia. Vilevile ukatili na uhalifu huu umefanyika chini ya kimya cha jamii ya kimataifa na uungaji mkono na misaada ya nchi kama Marekani zinazoendelea kuzihami na kizikingia kifua nchi waitifaki na vamizi katika vita vya Yemen.       

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*