?>

UN: Watoto 75 wameuawa Myanmar, 1000 wanashikiliwa tangu jeshi litwae madaraka ya nchi

UN: Watoto 75 wameuawa Myanmar, 1000 wanashikiliwa tangu jeshi litwae madaraka ya nchi

Kamati ya Watoto ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, watoto wasiopungua 75 wameuawa nchini Myanmar na watu wapatao 1,000 wanashikiliwa kizuizini tangu jeshi la nchi hiyo lilipotwaa kwa nguvu madaraka ya nchi miezi kadhaa iliyopita.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mikiko Otani, Mwenyekiti wa Kamati ya Watoto ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa, wamepokea taarifa za kusikitisha kuhusiana na hali mbaya wanayokabiliwa nayo watoto huko nchini Mynamr tangu jeshi lilipochukua madaraka.

Baadhi ya watoto nchini humo wamekuwa wakitiwa mbaroni kiholela na kushikiliwa katika vituo vya polis, jela au katika vituo vya jeshi, imeongeza taarifa hiyo ya Kamati ya Watoto ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi Februari Mosi mwaka huu baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo.

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai yake ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

Licha ya malalamiko ya kieneo na kimataifa na miito inayotolewa, jeshi la Myanmar limekataa kabisa kukabidhi madaraka ya nchi kwa utawala wa kiraia na hivyo kuiweka nchi hiyo katika mazingira magumu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*