?>

UN yataka kuwasilishwa nyaraka zinazoonyesha kuwa hai binti ya mtawala wa Dubai

UN yataka kuwasilishwa nyaraka zinazoonyesha kuwa hai binti ya mtawala wa Dubai

Kamishna wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ameutaka Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) uwasilishe nyaraka zinazoonyesha kwamba Mwanamfalme Latifa binti wa mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed Al Maktoum yuko hai na salama salimini.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Umoja wa Mataifa jana uliwataka viongozi wa Imarati wawasilishe nyaraka au ishara yoyote inayooonyesha kuwa hai binti huyo wa mtawala wa Dubai. 

Kwa mujibu wa ripoti ya United Press, ombi hilo la Umoja wa Mataifa limetolewa wiki moja baada ya mwanamfalme huyo Latifa binti wa mtawala wa Dubai kutuma ujumbe kwa njia ya video akieleza kuwa ametekwanyara na familia yake.  

Ofisi ya Michel Bachelet Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa pia imetangaza kuwa umoja huo unaitaka familia ya mwanamfalme Latifa Mohammed Al Makhtoum ionyeshe vithibitisho vinavyoashiria kuwa hai na salama binti huyo. Elizabeth Trussell Msemaji wa bi Bachelet jana Ijumaa aliwaambia waandishi wa habari huko Uswisi kwamba, kwa kuzingatia video yenye kutia wasiwasi waliyoiona wanataka kupatiwa taarifa na maelezo ya wazi kuhusu hali ya Sheikha Latifa. 

Sheikha Latifa aliye na umri wa miaka 34 mwaka 2018 alijaribu kutoroka Imarati kupitia njia ya bahari kwa kusaidiwa na afisa mmoja wa zamani wa intelijinsia wa Ufaransa ambaye alikuwa akimsubiri katika boti, hata hivyo makomando walifanikiwa kumkamata binti huyo wa mtawala wa Dubai katika pwani ya maeneo ya India. Dada wa Latifa amethibitisha kuwa ndugu yake amefungwa huko Dubai. Ameongeza kuwa Latifa  yupo chini ya ulinzi wa askari wa baba yake huku wakimpa madawa ya kulevya.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni