?>

UN: Yemen inasumbuliwa na mgogoro mbaya zaidi wa binadamu duniani

UN: Yemen inasumbuliwa na mgogoro mbaya zaidi wa binadamu duniani

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu amesema kuwa, Yemen inasumbuliwa na maafa ya binadamu na kwamba kwa sasa nchi hiyo inapita katika mgogoro mbaya zaidi uliowahi kushuhudiwa duniani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mark Lowcock amesema thuluthi mbili ya watu wa Yemen wanahitajia misaada ya dharura na kwamba, njia pekee ya kupata suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo ni mchakato wa mazungumzo ya amani.

Awali Umoja wa Mataifa ulikuwa umetangaza kuwa, nchi ya Yemen inasumbuliwa na mgogo mkubwa zaidi wa chakula duniani. 

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, UAE na nchi zingine kadhaa iliivamia Yemen na kuiwekea mzingiro wa nchi kavu, baharini na angani ambao unaendelea hadi sasa.

Vita hivyo vya Saudia vimesababisha maafa makubwa zaidi ya binadamu nchini Yemen.

Kwa mujibu  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Idadi kubwa ya raia hasa wanawake na watoto ni waathirika wakuu wa hujuma za Saudia dhidi ya Yemen.

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kati ya Januari na Juni 2021, asilimia 54 ya Wayemen, yaani watu milioni 16.2, watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vya Saudia dhidi ya nchi hiyo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*