?>

Unesco: Corona changamoto kubwa zaidi iliyoyumbisha sekta ya elimu katika historia

Unesco: Corona changamoto kubwa zaidi iliyoyumbisha sekta ya elimu katika historia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) ametahadharisha juu ya hatari zilizosababishwa na maambukizi ya kirusi cha corona na kupelekea kufungwa skuli duniani kote.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Audrey Azoulay Mkurugenzi Mkuu wa Unesco ameeleza kuwa, maambukizi ya corona yameathiri pakubwa sekta ya elimu duniani kuwahi kushuhudiwa katika historia na kuongeza kuwa: maambukizi ya corona yamesababisha kufungwa skuli na Vyuo Vikuu kote duniani; na kupelekea kuongezeka pakubwa ukosefu wa usawa katika elimu na kuleta mabadiliko ya msingi ambayo yameathiri mfumo mzima wa elimu.  

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Unesco ameongeza kuwa, kufungwa skuli na Vyuo Vikuu kwa muda mrefu kunazidi kupunguza kiwango cha kujifunza na kuathiri zaidi afya ya akili ya wanafunzi.  

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Unesco inafanya juhudi kuendelea kutoa elimu kwa njia yoyote ikiwemo kutoa elimu kupitia mawasiliano ya mbali yenye uhakika; japokuwa haiwezi kuwa mbadala wa elimu ya uhudhuriaji darasani. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni