?>

UNESCO: Mauaji ya waandishi habari yalipungua 2021, lakini vitisho vingalipo

UNESCO: Mauaji ya waandishi habari yalipungua 2021, lakini vitisho vingalipo

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limetangaza kuwa, waandishi wa habari 55 waliuawa katika mwaka uliopita 2021,

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti hiyo inaeleza kuwa theluthi mbili ya mauaji hayo yalifanyika katika nchi ambazo hazikukumbwa na migogoro ya silaha, ikionesha hatari wanazoendelea kukabiliana nazo waandishi wa habari katika ripoti zao za kila siku kufichua makosa.

Hii inaashiria kurejea nyuma kwa hali hiyo miaka michache tu iliyopita, mwaka 2013, wakati theluthi mbili ya mauaji yalifanyika katika nchi zenye migogoro.

Hata hivyo licha ya kiwango cha  mauaji  dhidi waandishi wa habari kupungua, lakini ukandamizaji na vitisho vimeendelea kuwa, changamoto kubwa katika utendaji kazi wa waandishi wa habari katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ameeleza kuwa "kwa mara nyingine tena mwaka wa 2021, wanahabari wengi sana walilipa gharama kubwa katika majukumu yao ya kuwafikishia ukweli walimwengu. Hivi sasa, ulimwengu unahitaji habari huru, za ukweli zaidi kuliko hapo awali. Ni lazima tufanye mengi zaidi ili kuhakikisha kwamba wale wanaofanya kazi bila kuchoka kufanikisha hilo wanaweza kufanya hivyo bila woga."   

Sehemu nyingine ya ripoti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) imebainisha kuwa, waandishi wa habari duniani kote pia wanaendelea kukabiliwa na viwango vya juu vya kufungwa, kushambuliwa kimwili, vitisho na unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na wakati wa kufuatilia maandamano.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*