?>

UNHCR: Hali ya wakimbizi wa Eritrea huko Tigray inatia wasiwasi

UNHCR: Hali ya wakimbizi wa Eritrea huko Tigray inatia wasiwasi

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR ) amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa juu ya hali ya wakimbizi wa Eritrea katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa yake iliyotolewa mjini  Geneva, Uswisi, Filippo Grandi amesema “tangu kuzuka kwa mapigano kwenye jimbo hilo la Tigray mwezi Novemba mwaka 2020, wakimbizi hao kutoka Eritrea wameathirika sana na ghasia na ukosefu wa usalama ambao umelikumba ene hilo. 

Aidha amesema, wakimbizi hao wamekuwa katikati ya makundi yanayokinzana huku kambi zao mbili zikiwa zimeteketezwa kabisa na makumi ya maelfu ya wakimbizi wa Eritrea wamelazimika kukimbia tena.”

Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) amesema pia kuwa, wamepokea taarifa za uhakika za mashambulizi ya kulipiza kisasi, kukamatwa, kutekwa nyara na ghasia dhidi ya wakimbizi hao wa kutoka Eritrea kwa madai ya kuhusika kwao kwenye upande mmoja wakati wote wa mapigano hayo yaliyosababisha umwagaji wa damu.

Serikali ya Ethiopia ilianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya eneo la Tigray Novemba mwaka jana, kwa madai kuwa wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) wamelishambulia jeshi la nchi hiyo na kuwaua askari waliokuwa wamelala na kupora zana zao za kijeshi.

Mwisho wa wiki iliyopita, Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia - ambayo ni chombo huru - ilielezea wasiwasi wake mkubwa juu ya kukamatwa waandishi wa habari, ikisisitiza kwamba mahabusu hao wamenyimwa haki ya kukutana na wanasheria na familia zao.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*