?>

UNICEF: UVIKO-19 imezidi kuwatia hatarini watoto wadogo duniani

UNICEF: UVIKO-19 imezidi kuwatia hatarini watoto wadogo duniani

Janga la UVIKO-19 (COVID-19) limezidi kuwaweka kwenye hatari watoto wengi duniani, wengi wao wakiwa ni wale waliopoteza wazazi wao na sasa wako katika hatari ya kutumbukia kwenye hali ngumu na mbaya kwa kukosa walezi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema hayo katika ripoti yake ya jana Jumatatu na kuongeza kuwa, watoto wengi walioko katika hatari ya madhara ya janga la UVIKO-19 ni wale wenye matatizo ya kupoteza wazazi wao kutokana na vifo, magonjwa na matatizo makubwa ya fedha.

Ripoti hiyo ya Mkurugenzi Mtendani wa UNICEF, Henrietta Fore imeongeza kuwa, kadiri janga la corona lianvyoendelea, ndivyo wajibu wa kusaidia familia maskini na watoto waliopoteza wazazi wao unavyozidi kuwa mkubwa. 

Ripoti hiyo ya Fore imetolewa katika hali ambayo watu waliopoteza maisha duniani kwa ugonjwa wa UVIKO-19 imeshapindukia milioni 4 huku vifo zaidi vikiendelea kuripotiwa kila leo katika kila kona ya dunia.

Siku chache zilizopita pia, UNICEF ilitangaza kuwa, imenuia kutuma dozi milioni 220 za chanjo ya kirusi cha UVIKO-19 (COVID-19) au corona kwa nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022. 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeongeza kuwa, limesaini makubaliano na shirika moja la kimataifa   la Janssen Pharmaceutica NV  mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya kuteeneza chanjo za kutumwa barani Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Henrieta Fore alisema kuwa, nchi za Afrika zinapaswa kupata chanjo ya  UVIKO-19 kwa usawa na kwa gharama nafuu haraka iwezekanavyo. Alisema mpaka sasa ni asilimia moja tu ya watu barani Afrika ambao wamepata chanjo hiyo mpaka sasa.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*