?>

UNICEF: Watoto 371,504 wamezaliwa Januari 1 duniani kote

UNICEF: Watoto 371,504 wamezaliwa Januari 1 duniani kote

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekadiria katika siku ya kwanza ya mwaka huu wa 2021, watoto 371,504 wamezaliwa kote ulimwenguni.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa makadirio hayo ya UNICEF, zaidi ya nusu ya "watoto wa Mwaka Mpya" wamezaliwa katika nchi kumi zifuatazo: India (takriban 59,995), Uchina (35,615), Nigeria (21,439), Pakistan (14,164), Indonesia (12,336), Ethiopia (10,206), Marekani (10,312), Misri (9,455), Bangladesh (9,236), na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC (8,640).

Aidha  kwa mujibu wa uchunguzi wa sensa ya kitaifa na data ya usajili, na pia ripoti ya Umoja wa Mataifa ya "Mtazamo wa Idadi ya Watu", UNICEF inakadiria kuwa jumla ya takriban watoto milioni 140 watazaliwa ulimwenguni mnamo 2021, wakiwa na wastani wa umri wa kuishi wa miaka 84.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore anasema, "watoto waliozaliwa Siku ya Mwaka Mpya wamekuja kwenye ulimwengu tofauti kabisa na mwaka mmoja uliopita." Kwa mustakabali wa watoto hawa, ametaka jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja akisema, "ufanye mwaka 2021 uwe aina ya Mwaka wa haki zaidi, salama na afya kwa watoto."

Bi Fore ameongeza kusema, "wakati ulimwengu unakabiliwa na janga jipya la corona, kushuka kwa uchumi, kuongezeka kwa umaskini, na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kazi ya UNICEF ni muhimu zaidi kuliko hapo awali."

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*