?>

Usitishaji vita; igizo la usanii inaofanya Saudia Yemen kwa kuutumia vibaya Umoja wa Mataifa

Usitishaji vita; igizo la usanii inaofanya Saudia Yemen kwa kuutumia vibaya Umoja wa Mataifa

Awamu ya kwanza ya ubadilishanaji mateka kati ya Yemen na Saudi Arabia imefanyika katika hali ambayo Riyadh ingali inazuia kufunguliwa tena Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana'a.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hans Grundberg, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen alitangaza usitishaji vita wa muda wa miezi miwili katika vita vya Yemen, ambao ulianza kutekelezwa tarehe Pili ya mwezi uliopita wa Aprili. Siku 36 zimepita tangu usitishaji huo wa mapigano ulipoanza kutekelezwa. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Grundberg, pande mbili hasimu zilikubaliana kuhusu kuingia meli za fueli katika bandari ya Al-Hudaydah magharibi ya Yemen, kubadilishana mateka wa vita pamoja na kufanyika safari za ndege za kibiashara za kuingia na kutoka uwanja wa ndege wa Sana'a kuelekea viwanja maalumu vya ndege katika eneo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*