?>

Utawala wa Al Khalifa Bahrain unatumia mbinu ya utesaji kuzima mgomo wa wafungwa wanaosusia kula

Utawala wa Al Khalifa Bahrain unatumia mbinu ya utesaji kuzima mgomo wa wafungwa wanaosusia kula

Vikosi vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa vimepanga kutumia nguvu na utesaji dhidi ya wafungwa Wabahrain sambamba na kuwapiga na kuwatusi ili kuzima mgomo wa kususia kula ulioanzishwa na wafungwa hao.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu ameeleza katika ripoti yake mpya kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Bahrain kwamba, katika mbinu ya utesaji wanayotumia dhidi ya wafungwa waliosusia kula, askari wa usalama wa utawala wa Aal Khalifa wanawafyatulia wafungwa hao risasi zenye mlio mkali unaoathiri masikio.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vikosi vya usalama vya utawala wa Manama vinatumia mbinu kali kabisa za ukatili na utumiaji nguvu dhidi ya wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika mahabusu ya Jaw, huku wakiwapiga na kuwatusi ili kuhakikisha wanazima mgomo wa kususia kula ulioanzishwa na idadi kadhaa ya wafungwa tangu tarehe 5 ya mwezi uliopita wa Aprili.

Wafungwa Wabahrain wanaoshikiliwa kwenye jela hiyo wameanzisha mgomo wa kususia kula kulalamikia kukamatwa kwa Abbas Maalullah, mwanaharakati wa kisiasa, ambaye aliaga dunia baada ya kunyimwa huduma za matibabu.

Marta Hurtado, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu alisisitiza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, kamishna wa haki za binadamu Michelle Bachelet anasikitishwa sana na utumiaji nguvu na ukatili unaofanywa na askari usalama na polisi wa Bahrain kwa ajili ya kuzima mgomo katika jela ya nchi hiyo.

Tangu Februari 14, 2011 hadi sasa, Bahrain imekuwa uwanja wa mapambano ya amani ya wananchi dhidi ya utawala wa kiimla wa Aal Khalifa; na tangu wakati hadi sasa raia zaidi ya 11,000 wametiwa nguvuni kwa tuhuma bandia na idadi kubwa ya wapinzani wa utawala huo wa kifamilia wamevuliwa uraia.../ 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*