?>

Uturuki yalaani uamuzi wa Mahakama ya Ulaya wa kuruhusu marufuku ya vazi la hijabu

Uturuki yalaani uamuzi wa Mahakama ya Ulaya wa kuruhusu marufuku ya vazi la hijabu

Uturuki imelaani uamuzi wa Mahakama ya Jumuiya ya Ulaya wa kuruhusu marufuku ya vazi la hijabu katika hali fulani, na kuutaja uamuzi huo kuwa ni "ukiukaji wazi wa uhuru wa kidini".

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Uturuku imesema kuwa uamuzi huo utazidisha chuki na uhasama dhidi ya wanawake wa Kiislamu barani Ulaya.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema kuwa, uamuzi huo ni ishara ya kuongezeka vita na propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika kipindi hiki ambapo wanawake wa Kiislamu wanasumbuliwa na ubaguzi kwa sababu ya imani na itikadi zao za kidini.

Jumamosi iliyopita pia Mkurugenzi wa Ikulu ya Rais wa Uturuki, Fahrettin Altun alilaani uamuzi huo akisema ni jaribio la kuhalalisha ubaguzi.

Suala la vazi la staha la mwanamke wa Kiislamuu, hijabu, limezua utata katika nchi za Ulaya kwa miaka sasa, na kuonesha mgawanyiko mkubwa uliopo juu ya mchakato wa kujumuishwa Waislamu katika jamii za Ulaya.

Itakumbukwa kuwa Alhamisi iliyopita, Mahakama Kuu ya EU ilisema makampuni yanaweza kuwapiga marufuku wafanyikazi wa kike Waislamu kuvaa hijabu katika hali fulani iwapo makampuni hayo yanataka kuwasilisha picha ya kutopendelea upande wowote kwa wateja.

Vilevile mwaka 2017 Mahakama ya Haki ya Ulaya (ECJ) yenye makao yake huko Luxembourg ilipasisha marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu.

Hiyo ilikuwa hukumu ya kwanza kutolewa na mahakama ya Ulaya kuhusu mjadala wa vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu katika maeneo ya kazi.

Wimbi kubwa la propaganda chafu za kupiga vita Uislamu na Waislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi limeisababishia vizingiti vingi na mbinyo mkubwa jamii ya Waislamu barani Ulaya.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*