?>

Uvamizi na vita vya miaka 20 vya Afghanistan vimeigharimu Marekani dola trilioni mbili

Uvamizi na vita vya miaka 20 vya Afghanistan vimeigharimu Marekani dola trilioni mbili

Ripoti iliyotolewa na kanali ya televisheni ya ABC News ya Marekani imeeleza kuwa, uvamizi wa kijeshi na vita vya miaka 20 vilivyoanzishwa na Marekani nchini Afghanistan vimegharimu takriban dola trilioni mbili na vifo vya watu wapatao laki moja na 20 elfu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Waafghanistan ndio waliotahirika zaidi kutokana na vita na mapigano yaliyotokea nchini mwao.

Utafiti uliofanywa chini ya anuani ya "Gharama ya Vita" na chuo kikuu cha Brown cha nchini Marekani unaonyesha kuwa, kuanzia mwaka 2001 hadi katikati ya Aprili 2021, raia wasiopungua 47,245 wa Afghanistan wameuawa kutokana na vita na mapigano nchini humo.

Kwa muijibu wa utafiti huo, waandishi 72 wa habari na wafikishaji misaada ya kibinadamu 444 wameuawa pia katika vita na mapigano hayo.

Askari zaidi 66,000 wa Afghanisitan wameuawa pia katika vita vya nchi hiyo.

Ripoti hiyo ABC News imebainisha pia kuwa, watu wapatao milioni nne wamebaki bila makazi nchini Afghanistan kutokana na vita na uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imetangaza kuwa tangu mwaka 2001 hadi sasa askari 2,442 wa nchi hiyo wameuawa na wengine zaidi ya 20,500 wamejeruhiwa katika vita vya Afghanistan.

Vita na mapigano hayo vimepelekea kuuawa pia askari 1,144 wa nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO.

Rais Joe Biden wa Marekani alitangaza hivi karibuni kuwa, hadi ifikapo Septemba 11, 2021, askari wa nchi hiyo watakuwa wameshaondoka katika ardhi ya Afghanistan.

Mnamo mwaka 2001, Marekani na waitifaki wake waliishambulia na kuivamia kijeshi Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha amani nchini humo; hata hivyo uvamizi huo uliitumbukiza Afghanistan kwenye lindi la vita na mapigano, kuangamiza miundomsingi yake ya kiuchumi  na kushamirisha machafuko, ugaidi na uzalishaji wa madawa ya kulevya katika nchi hiyo.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*