?>

Vifo vya corona nchini Marekani vyakaribia watu 394,000

Vifo vya corona nchini Marekani vyakaribia watu 394,000

Mtandao wa Worldmeters unaotoa takwimu za kila sekunde za ugonjwa wa COVID-19 umetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kwa cona nchini Marekani hadi leo asubuhi kulingana na takwimu rasmi zinazotolewa na serikali ya nchi hiyo ni 393,928.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mtandao huo aidha umeripoti leo asubuhi kwamba, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 nchini Marekani kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali ni milioni 23 na 616,345. Kati ya hao 393,928 wameshapoteza maisha ikiwa na maana kwamba katika kila dakika 3 Mmarekani mmoja hufariki dunia kwa corona kila siku.

Katika siku ya Jumanne pekee, Marekani ilisajili vifo vya watu 4,470 waliofariki dunia kwa COVID-19 ikiwa ni rekodi mpya iliyovunja rekodi ya huko nyuma iliyokuwa imewekwa pia na Marekani.

Sasa hivi Marekani inaongoza kwa mbali duniani katika upande wa idadi ya wagonjwa na vifo vinavyotokana na corona na lawama kubwa zinaelekezwa kwa serikali ya Donald Trump ambayo imezembea na kulidharau mno, bali hata kulifanyia istihzai janga hilo la dunia nzima.

Serikali ya Marekani ilicherewa mno kuchukua tahadhari, kupima na kuweka sheria za kujikinga na ugonjwa huo. Sasa hivi imekumbwa na upoungufu mkubwa wa vifaa vya matibabu kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa corona.

Janga jingine lililoikumba Marekani mbali na kuongoza kwake dunia kwa idadi kubwa ya wagonjwa na vifo vya corona, ni mgogoro mkubwa wa kuizika miili ya wagonjwa wanaofariki kwa COVID-19 katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. Sasa hivi Marekani imeamua kuwazika wahanga wa corona katika makaburi ya umati kutokana na uchache wa maeneo ya kuzikia.

Donald Trump na serikali yake wanalaaniwa vikali na wananchi wa Marekani kwa kuwasababishia janga kubwa kwa uzembe na ubishi wao. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni