?>

Vikosi vya Yemen vimeidhibiti jela yenye mfungamano na Mansour Hadi huko Ma'rib

Vikosi vya Yemen vimeidhibiti jela yenye mfungamano na Mansour Hadi huko Ma'rib

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imetengakuwa, jeshi la Yemen na harakati ya Ansarullah vimeidhibiti jela ya wanamgambo wenye mfungamano na Mansour Hadi Rais wa Yemen aliyejiuzulu. Jela hiyo imedhibitiwa huko katika mji wa Ma'rib.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya al Mayadeen imeripoti kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndan ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen jana Jumatatu ilitangaza kuwa jeshi na harakati ya Ansarullah ya nchi hiyo imewaachia huru mateka 9 baada ya kuidhibiti jela hiyo ambao mamluki wa muungano vamizi walikuwa na lengo la kuwakabidhi kwa wanajeshi wa Saudia. 

Duru za kieneo katika mkoa wa Ma'rib pia zimetangaza kuwa, jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen jana yalipigana vikali na wanajeshi wa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia na kufanikiwa kusonga mbele kutoka upande wa kaskazini na kuelekea mashariki mwa mji wa Ma'rib. 

Kusonga mbele huko kwa vikosi vya Yemen katika mkoa wa Ma'rib kumeupelekea muungano vamizi waSaudia kulazimika kutuma zaidi wanajeshi katika eneo hilo. 

Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine zinazouunga mkono muungano huko vamizi wa Saudia huko Yemen pia zimetoa pendekezo la kuistisha vita kwa serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen hata hivyo serikali hiyo imepinga pendekezo hilo kutokana na muungano vamiz kutosimamisha mashambuliziyake huko Yemen. Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imesema muungano mashambulizi na mzingiro dhidi ya Yemen vinapaswa kusitishwa kikamilifu kama sharti la kukubaliwa pendekezo hilo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni