?>

Vikosi vya Yemen vyafanya shambulio la kushtukiza dhidi ya jeshi la Saudia huko Najran

Vikosi vya Yemen vyafanya shambulio la kushtukiza dhidi ya jeshi la Saudia huko Najran

Duru za habari zimeripoti kuwa vikosi vya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi vimefanya shambulio la kushtukiza dhidi ya wanajeshi wa Saudi Arabia kusini mwa Saudia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA:Televisheni ya al Masira imetangaza kuwa, Kitengo cha Upashaji Habari za Kivita chenye mfungamano na jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen kimetangaza kuwa vikosi vya Yemen vimetekeleza oparesheni na kutoa pigo kali kwa askari jeshi wa Saudia baada ya kuzitambua kwa makini ngome na maeneo ya wanajeshi hao.  

Wakati huo huo chumba cha oparesheni za maafisa wanajeshi wa Yemen kimeripoti kuwa, adui Msaudia amekiuka mapatano ya usitishaji vita ya al Hodeidah mara 152 kwa kutekeleza oparesheni za makombora na kukiuka anga ya Yemen. 

Jeshi la Yemen limeripoti kuwa, wanajeshi vamizi wa Saudia wameyashambulia mara nne kwa ndege za kivita maeneo mbalimbali  huko al Durayhimi. Aidha ndege za kijasusi za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia huko Yemen zimeruka katika maeneo ya al Fazah, al Jabaliyah, al Haj na al Tahita na kukusanya taarifa za ujasusi. Vikosi vamizi vya Saudia pia vimeyashambulia kwa makombora mara 20 maeneo yaliyoko katika mpaka wa Yemen huku mamluki wa nchi hiyo wakifyatua risasi mara 120 kuelekea katika maeneo ya jeshi na raia katika miji ya mpakani huko Yemen. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*