?>

Vita ya Maʼrib, muungano wa Saudi Arabia na Daesh na jitihada za kukimbia kinamasi cha Yemen

Vita ya Maʼrib, muungano wa Saudi Arabia na Daesh na jitihada za kukimbia kinamasi cha Yemen

Sambamba na kuendelea kusonga mbele wapiganaji wa makundi ya kujitolea ya Yemen kuelekea Maʼrib, Saudi Arabia imeamua kutuma askari wa ziada nchini Yemen na kutumia wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh huku nchi za Kiarabi zikifanya juhudi kubwa za kidiplomasia za kuzuia fedheha na kushindwa Riyadh na waitifaki wake katika kinamasi cha Yemen.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mwezi mmoja ujao vita vya Saudia dhidi ya taifa la Yemen vitakuwa vimekamilisha miaka sita. Hadi sasa tayari nyaraka za historia zimesajili kushindwa na kufedheheka kwa Saudia na waitifaki wake wa Kimagharibi katika vita hivyo. Moja kati ya sababu za uamuzi wa Rais Joe Biden wa Marekani wa kusitisha misaada na himaya yake kwa Saudia na washirika wake katika vita vya Yemen ni kukiri kwamba muungano huo umefeli katika medani za vita.

Kwa sasa Maʼrib iliyoko katikati mwa Yemen ndio uwanja mkuu wa mapigano na vita. Katika siku za karibuni wapiganaji wa Yemen wamefanikiwa kukomboa kilomita mraba karibu 35 za mji wa Sirwah ambao unatajwa kuwa mji mkubwa zaidi wa mkoa wenye utajiri mkubwa wa mafuta wa Maʼrib. Sasa jeshi na wapiganaji wa harakati ya wananchi ya Ansarullah wako umbali wa kilomita 10 tu kutoka katikati ya mkoa huo. Maendeleo hayo yameitia kiwewe na wahka mkubwa Saudi Arabia ambayo imeanzisha harakati mpya za kuepeka fedheha zaidi. 

Shirika la habari la Reuters limetangaza kuwa, maafisa wa serikali iliyojiuzulu na kukimbilia Saudi wamelitaarifu shirika hilo kwamba, mamia ya wanajeshi wa muungano wa Saudi Arabia wamepelekwa eneo na Maʼrib wakitokea mikoa ya Shabwah na Hadhramaut huko kusini mwa Yemen na vilevile kandokando ya mkoa wa Sana'a huko kaskazini mwa Yemen. Wakati huo huo wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wametangaza kuwa wanashiriki katika operesheni za kijeshi na vita dhidi ya Ansarullah katika eneo la Maʼrib. Kwa maneno mengine ni kuwa, Saudi Arabia imeamua kuliomba msaada kundi la kigaidi la Daesh ili kuepuka fedheha na kushindwa zaidi katika vita vya Maʼrib. 

Sambamba na hatua hizo za kijeshi, waitifaki wa Saudia wameanzisha harakati kubwa ya kidiplomasia. Aal Saudi wameipigia magoti Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, Martin Griffiths wakitaka kuzidishwa mashinikizo ya kusitishwa vita huko Ma'rib. 

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen, Muhammad Ali al Houthi amejibu wito wa mjumbe maalumu wa UN katika masuala ya Yemen wa kusitishwa vita katika mkoa wa Maʼrib akisema: Vita hivi vimekuwa vikiendelea tangu baada ya kufeli mashambulizi ya majeshi vamizi katika eneo la Nihm, sasa inakuwaje Griffiths anavitaja kuwa ni shambulizi jipya dhidi ya Maʼrib?

Idara ya Siasa ya harakati ya Ansarullah pia imepinga msimamo wa baadhi ya nchi unaoupendelea muungano vamizi wa Saudi Arabia kuhusiana na hali ya mambo huko Maʼrib ikisema: "Misimamo hiyo kuhusu yanayojiri Maʼrib haifai na ni mwavuli wa kuendeleza uvamizi na kuizingira nchi ya Yemen."

Haya yote na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya Saudi Arabia vinaonyesha umuhimu mkubwa wa eneo hilo la Maʼrib kwa muungano huo vamizi. Hii ni kwa sababu, mbali na kwamba, Maʼrib ni mkoa wenye utajiri mkubwa wa mafuta na kudhibiti mkoa huo kunaweza kuisaidia sana Serikali ya Uokovu wa Kitaifa katika upande wa uchumi, lakini pia ushindi katika eneo hilo utakuwa na maana ya kushindwa kikamilifu Wasaudia katika vita vya Yemen. 

Mkoa wa Maʼrib ambao ni maarufu kwa jina la "Moyo wa Yemen", uko umbali wa kilomita karibu 170 kutoka Sana'a. Muungano vamizi wa Saudia ulikuwa ukifanya jitihada za kudhibiti mkoa huo na hivyo kukaribia Sana'a na kuzuia ushawishi na mafanikio zaidi ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa nchini Yemen. 

Kwa msingi huo inatupasa kusema kuwa, kushindwa muungano vamizi wa Saudia huko Maʼrib ni mafanikio makubwa na ushindi wa kistratijia kwa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen.   

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni