?>

Waafghani milioni 19.7 wanakabiliwa na njaa kali

Waafghani milioni 19.7 wanakabiliwa na njaa kali

Watu milioni 19.7, karibu nusu ya idadi ya watu wote wa Afghanistan, wanakabiliwa na njaa kali kulingana na ripoti ya uchambuzi wa hivi karibuni wa tathimini ya hali ya uhakika wa chakula (IPC) iliyofanywa mwezi Januari na Februari 2022.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tathmini hiyo imefanywa na washirika wa masuala ya chakula na kilimo, ikiwa ni pamoja na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali au NGOs. 

Ripoti hiyo inatabiri kuwa mtazamo wa Juni hadi Novemba 2022 unaonesha kuboreka kidogo kwa hali ya uhakika wa chakula, na kupungua kwa idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hadi kufikia watu milioni 18.9.  

Hii inatokana kwa kiasi fulani na mavuno ya ngano yanayofanyika kuanzia mwezi huu wa Mei hadi Agosti, na uratibu mzuri wa mwaka huu wa upanuzi wa wigo wa msaada wa kibinadamu wa chakula pamoja na kuongezeka kwa msaada wa maisha ya kilimo. Hata hivyo, faida itakuwa ndogo inaonya ripoti hiyo. Ukame unaoendelea na mzozo mkubwa wa kiuchumi unamaanisha kuwa njaa isiyo na kifani itaendelea kutishia maisha ya mamilioni ya watu kote Afghanistan. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*