?>

Waasi wa Chad watishia kujiondoka katika mazungumzo ya amani ya Doha

Waasi wa Chad watishia kujiondoka katika mazungumzo ya amani ya Doha

Waasi wa Chad wanaofanya mazungumzo na Baraza la Kijeshi linalotawala nchi hiyo huko Qatar wametishia kujiondoka katika mazungumzo ya amani.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Makundi ya waasi nchini Chad yametoa taarifa yakiwashutumu maafisa wa serikali kwamba wanashirikiana na mamluki na kuhujumu mazungumzo kwa njia ya vitisho, uchochezi na ubakaji.

Taarifa hiyo imesema: "Makundi haya yana haki ya kusimamisha au kujiondoa katika mazungumzo." Yamesisitiza kuwa amani itapatikana nchini Chad iwapo serikali itatekeleza majukumu yake kikamilifu.

Pande zinazoshiriki katika mazungumzo ya Doha zina matumaini kuwa mazungumzo hayo yatapanuka zaidi na kuzishirikisha pande zote, wapinzani wa kisiasa na makundi yenye silaha na kwamba katiba mpya itaandikwa kwa mujibu wa matokeo ya mazungumzo hayo.

Mazungumzo ya amani yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu ya Chad yalianza tarehe 13 mwezi Machi mjini Doha yakiwashirikisha wawakilishi wa jeshi linalotawala na makundi ya waasi.

Mazungumzo hayo yanaelezwa kuwa ni hatua muhimu ya kuhitimisha uasi nchini Chad na kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi. Jumla ya makundi 44 ya waasi yamealikwa kushiriki katika mazungumzo hayo.

kwa sasa Chad inaongozwa na wanajeshi wanaoshika hatamu za uongozi baada yya kifo cha Rais Idriss Déby.

Deby ambaye aliiongoza Chad kwa kipindi cha miaka 30, aliuawa kabla ya kuapishwa kuingoza nchi hiyo kwa awamu ya sita baada ya Kamisheni ya Uchaguzi kumtangaza mshindi. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*