?>

Wabahrain waandamana kupinga kuteuliwa balozi wa Israel nchini humo

Wabahrain waandamana kupinga kuteuliwa balozi wa Israel nchini humo

Wananchi wa Bahrain jana Ijumaa walimiminika mabarabarani kushiriki maandamano ya kulaani uteuzi wa balozi mdogo wa utawala haramu wa Israel katika nchi hiyo ya Kiarabu, huo ukiwa ni muendelezo wa hatua za kuimarisha uhusiano baina ya Manama na Tel Aviv.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mara nyingine tena, wananchi hao wa Bahrain wamelaani vikali hatua ya watawala wa nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni. Kadhalika waandamanaji hao wametumia maandamano hayo kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.

Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao wa Bahrain yalikuwa na ujumbe unaosema "Wazayuni maghasibu, hakuna nafasi yenu katika ardhi yetu! Tutakutimueni."

Maandamano hayo yamefanya baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel kuandika katika katika mtandao wa Twitter ujumbe kwa lugha ya Kiarabu unaosema: Itay Tagner ameteuliwa kuwa balozi mdogo wa Israel mjini Manama na tayari ameshakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Al Khalifah.

Mwezi uliopita wa Disemba, Gabi Ashkenazi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala dhalimu wa Israel alinukuliwa akisema kuwa, muda si mrefu atafanya safari mjini Manama, Bahrain kwa ajili ya kwenda kufungua ubalozi wa utawala huo ghasibu katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 15 Septemba mwaka uliopita, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walitia saini makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya nchi zao na utawala ghasibu wa Israel.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Ikulu ya Marekani, White House, zilihudhuriwa pia na Rais wa Marekani, Donald Trump na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala katili wa Israel.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni