?>

Wabunge wa Somalia wapitisha kwa kauli moja uamuzi wa kurejesha upigaji kura wa uwakilishi

Wabunge wa Somalia wapitisha kwa kauli moja uamuzi wa kurejesha upigaji kura wa uwakilishi

Baraza dogo la bunge la Somalia limepitisha kwa kauli moja uamuzi wa kurejesha makubaliano yaliyofikiwa Septemba mwaka jana yatakayoruhusu nchi hiyo kuendelea na utaratibu wa upigaji kura kwa njia ya isiyo ya moja kwa moja ya uwakilishi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Spika Mohamed Mursal alisema katika kikao kilichofanyika jana Jumamosi kuwa, wabunge 140 wameunga mkono kurejeshwa utaratibu wa awali wa upigaji kura.

Mwezi uliopita bunge la Somalia lilipiga kura kurefusha muhula wa uongozi wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, kwa muda wa miaka miwili na kuamua pia nchi hiyo iitishe chaguzi zake zijazo kwa kutumia mfumo wa kura moja kwa mtu mmoja unaohakikisha viongozi wanachaguliwa kwa kura za moja kwa moja za wananchi.

Hata hivyo uamuzi huo ulipingwa na seneti, waziri mkuu, viongozi wa upinzani na majimbo manne kati ya sita za serikali ya shirikisho ya Somalia na kusababisha mkwamo wa kisiasa nchini humo.

Akihutubia bunge hilo hapo jana muda mfupi kabla ya upigaji kura, Rais Mohamed, maarufu kwa lakabu ya Farmaajo aliwatolea mwito wabunge kuunga mkono uamuzi wa kurejesha makubaliano ya Septemba 2020.

Aidha alimuagiza Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble kuongoza mchakato wa maandalizi ya uchaguzi na kuhakikisha unafanyika katika anga ya amani na uthabiti.

Farmaajo aliwaomba pia viongozi wa upinzani kutoa mchango wao kuhakikisha amani inatamalaki nchini na hasa katika mji mkuu Mogadishu kwa kwa ajili ya manufaa ya watu wa Somalia, nchi na dini yao.

Mwezi Septemba mwaka jana, rais wa Somalia na majimbo ya shirikisho walikubaliana kuitisha uchaguzi wa uwakilishi kabla ya kumalizika muhula wake wa uongozi Februari 8 mwaka huu, ambapo wawakilishi maalumu wanaochaguliwa na wazee wa koo za nchi hiyo huteua wabunge, ambao nao humchagua rais.

Somalia haijawahi kuitisha uchaguzi wa kura za moja kwa moja za wananchi tangu mwaka 1969; na jitihada za kufanikisha zoezi hilo zimekuwa zikikwamishwa na matatizo ya usalama au kukosekana irada ya kisiasa...


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*