?>

Wanachama wa WHO wapinga kusiasishwa uchunguzi wa chanzo cha corona

Wanachama wa WHO wapinga kusiasishwa uchunguzi wa chanzo cha corona

Nchi wanachama katika Shirika la Afya Duniani (WHO) zimeafikiana kwamba suala la kuchunguza chanzo na asili ya virusi vya corona halipasi kuhusishwa na masuala ya kisiasa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Tovuti ya CGTN imeripoti kuwa, zaidi ya vyama mia tatu vya siasa na jumuiya na taasisi za nchi zaidi ya mia moja duniani zimetoa taarifa ya pamoja zikimtaka mkuu wa Shirika la Afya Duniani kupinga jaribio lolote la kuhusishwa uchunguzi wa chanzo cha corona na masuala ya siasa.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya chombo kimoja cha habari cha Marekani kuendeleza kampeni ya nchi hiyo kuhusu chanzo cha virusi vya corona na kudai kuwa, maabara moja ya serikali ya Washington imetoa ripoti iliyohitimisha kwamba, dhana ya kuvuja virusi hivyo kutoka kwenye mabara ya mji wa Wuhan huko China yumkini ikawa ya kweli, na kwamba kuna haja ya kufanyika uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo.

Itakumbukwa kuwa, Rais Joe Biden wa Marekani ameviamuru vyombo vya upelelezi vya nchi hiyo kumkabidhi ripoti kuhusu chanzo cha jinsi virusi vya corona ilivyoanza katika kipindi cha sku 90, na suala hilo limepewa mazingatio makubwa na Kongresi ya nchi hiyo. 

China inasema kuwa, kuanzisha tena mjadala juu ya chanzo cha virusi vya corona baada ya suala hilo kuchunguzwa na Shirika la Afya Duniani ni sehemu ya njama ya Washington ya kuzidisha mashinikizo dhidi ya Beijing.     

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*