?>

Wanajeshi 7, washirika 4 wa Burkina Faso wauawa katika shambulio la kigaidi

Wanajeshi 7, washirika 4 wa Burkina Faso wauawa katika shambulio la kigaidi

Wanajeshi saba wa Burkina Faso na washirika wao wanne wameuawa katika hujuma ya kigaidi huko Kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Jeshi la Burkina Faso limesema katika taarifa iliyotolewa leo Ijumaa kwamba wanajeshi saba na washirika wanne wa kikosi cha ulinzi wameuawa katika mashambulizi mawili ya kuvizia yaliyotekelezwa na "magaidi" Kaskazini na katikati ya nchi.

Mwezi uliopita takriban wanajeshi 12 na raia wanne waliojitolea kushirikiana na jeshi waliuawa katika shambulio lililolenga kituo cha jeshi Kaskazini mwa Burkina Faso.

Shambulizi hilo lililenga kikosi cha jeshi cha Namissiguima katika mkoa wa Sanmatenga, eneo la Centre-Nord.

Eneo la Kaskazini mwa Burkina Faso limekuwa likishuhudia mashambulizi ya kigaidi tangu 2015, ambapo zaidi ya watu 1,000 wameuawa na zaidi ya milioni 1 kukimbia makazi yao.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi inatawaliwa na wanajeshi tangu Januari mwaka huu kufuatia mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Roch Kabore.

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba ametangaza usalama kama moja ya vipaumbele vyake. Hata hivyo kuongezeka kwa mashambulizi nchini humo kumeripotiwa katika wiki za hivi karibuni.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*