?>

Wanajeshi 8 wa Togo wauawa katika hujuma ya kigaidi

Wanajeshi 8 wa Togo wauawa katika hujuma ya kigaidi

Hujuma ya kigaidi nchini Toge imepelekea askari 8 wa jeshi la nchi hiyo kuuawa na wengine 13 kujeruhiwa katika hujuma Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burkina Faso.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Serikali ya Togo imethibitisha kutokea kwa mauaji dhidi ya vikosi vyake, vinavyopambana na magaidi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mpaka sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na hujuma hiyo ambayo inaelezwa, kutekelezwa na kundi la watu zaidi ya sitini waliokuwa na silaha, wakiwa kwenye pikipiki. Makabiliano hayo yanaelezwa yalidumu kwa zaidi ya saa mbili, kabla ya Togo kutuma vikosi zaidi. 

Mwezi Novemba mwaka uliopita, wanajeshi wa Togo walizuia shambulio la kigaidi kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya shambulio la Jumatano. 

Wiki iliyopita, kulikuwa na mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi katika nchi za Afrika Magharibi waliokutana kujadili hali ya usalama katika êneo hilo ambalo limeendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, na ikabainika kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na matukio zaidi ya elfu tano ya kigaidi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 16. 

Hayo yanajiri wakati ambao, ripoti mpya kuhusu ugaidi duniani inasema aslimia 48 ya vifo vinavyotokana na ugaidi duniani vilikuwa eneo la kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika.  Aidha asilimia 41 ya watu waliouawa na magaidi wa ISIS au Daesh duniani walitoka eneo hilo la Afrika. Hali kadhalika taarifa zinasema operesheni za kigaidi katika eneo la Afrika mwaka 2021 zilisababisha hasara ya kiuchumi ya dola bilioni 171.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*