?>

Wanazuoni wa Kiislamu wataka sheria ya kupiga marufuku kutukanwa matukufu ya kidini

Wanazuoni wa Kiislamu wataka sheria ya kupiga marufuku kutukanwa matukufu ya kidini

Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa mwito wa kupasishwa sheria ya kujinaisha na kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya dini mbalimbali duniani.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Taasisi hiyo ya kidini yenye makao makuu yake Doha, mji mkuu wa Qatar imesema itatuma ujumbe wa wasomi wa Kiislamu kuzitembelea nchi za Waislamu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na midahalo kuhusu kushtadi kesi za kuvunjiwa heshima dini tukufu ya Kiislamu.

Taarifa ya IUMS imesema, taasisi hiyo ya kimataifa ya wanazuoni wa Kiislamu itaiomba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Umoja wa Mataifa zishinikize kupasishwa sheria ya kukabiliana na hatua yoyote inayovunjia heshima thamani na matukufu ya dini za Mbinguni.

Haya yanajiri wakati huu ambapo mataifa ya Kiislamu yanaendelea kulaani kitendo cha wanasiasa wa chama tawala nchini India cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu.

Kufuatia chokochoko hizo, Qatar, Kuwait na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ziliwaita mabalozi wa India katika nchi hizo, kulalamikia hatua hiyo ya kumvunjia heshima Bwana Mtume SAW.

Hivi karibuni pia, Mamosta Abdul Salam Karimi, Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya jamii za wachache nchini Iran sambamba na kulaani jinai ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Sweden alisema kuwa, leo hii jamii ya mwanadamu inahitajia mno amani, usalama, kuishi pamoja na utulivu, mantiki na kuheshimiana, na kwamba vitendo kama vilivyotokea huko Sweden ni uchochezi wa wazi wa vurugu na machafuko.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*