Mamia ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano katika mji mkuu Khartoum na mji wa Omdourman kulalamikia kifo cha kutatanisha cha mwanaharakati mmoja wa kisiasa.
Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Alam, maandamano hayo yamefanyika kufuatia kifo cha mwanaharakati mashuhuri wa nchi hiyo, anayefahamika kama Bahaullah al-Nuri.
Bahaullah al-Nuri aliripotiwa kutekwa na askari wa kikosi cha dharuru ya haraka wiki mbili zilizopita. Waandamanaji hao wametoa mwito wa kulipizwa kisasi cha mauaji ya mwanaharakati huyo.
Maziko ya mwanaharakati huyo wa kisiasa wa Sudan yamegeuka na kuwa maandamano makubwa ya kulaani mauaji yake. Mwili wa mwendazake unaonesha kuwa aliteswa vibaya kabla ya kuuawa.
Al-Nuri alikuwa mwanachama wa Kamati ya Muqawama wakati wa maandamano yalimuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al-Bashir.
342/