?>

Watalii wa kigeni waongezeka Iran, waingiza pato la dola bilioni 2.3

Watalii wa kigeni waongezeka Iran, waingiza pato la dola bilioni 2.3

Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sekta ya utalii inazidi kuimarika humu nchini ambapo katika kipindi cha mwaka moja uliopita watalii wa kigeni wametumia dola bilioni 2.5 wakiwa ndani ya Iran.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Ali Bahadori Jahromi, Msemaji wa Serikali ya Iran ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Taarifa za hivi punde kutoka mashirika ya kimataifa zinaoneysha kuwa sekta ya utalii nchini Iran ambayo ilishuka kwa asilimia 45 mwaka 2020 iliweza kustawi kwa asilimi 40 mwaka 2021."

Aidha amesema sekta ya utalii nchini Iran imechangia ongezeko la ajira kwa asilimia 5.1 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Baraza la Kimataifa la Utalii na Usafiri limetangaza hivi karibuni kuwa kwa ujumla utalii duniani ulistawi kwa asilimia 21 mwaka 2021.

Mwaka 2020 kutokana na vizingiti vya corona, sekta ya utalii ilipungua kwa asilimi 50 lakini mwaka 2021 baada ya kupunguzwa vizingiti vya corona sekta hiyo ilianza kustawi tena na pato lake kufika dola bilioni 1000.Mchango wa utalii katika uchumi wa Iran mwaka 2020 ulikuwa ni asilimia 3 na kiwango hicho kiliongezeka na kupindukia asilimia nne mwaka 2021. Kufuatia kuongezeka idadi ya watalii, sekta ya ajira nayo pia imeweza kustawi nchini Iran. 

Iran ni nchi yenye ustaarabu mkongwe na hivyo ina vivutio vingi vya kitalii kwa wapendao historia. Aidha Iran ina vivutio vingi ya Kiislamu hasa maeneo ya ziara ambayo hutumbelewa na Waislamu kama vile Haram Takatifu ya Imam Ridha AS mjini Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran na Haram Takatifu ya Bibi Maasuma katika mji wa Qum kusini mwa Tehran.

Misimu minne ya Iran pamoja na vivutio vya kimaumbile na kihistoria ni nukta ambazo zimeigeuza Iran kuwa pepo kwa watalii. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*