?>

Watoto 500 Waamerika asili walipoteza maisha katika shule za bweni za kanisa Marekani

Watoto 500 Waamerika asili walipoteza maisha katika shule za bweni za kanisa Marekani

Ripoti mpya imefichua kuhusu vifo zaidi ya 500 katika shule za bweni za kanisa ambazo kwa zaidi ya karne moja zilijaribu kuwaingiza watoto wa jamii za asili za Amerika katika jamii ya wakoloni wazungu.

Ripoti iliyotolewa Jumatano na Idara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ilibainisha vifo katika rekodi ya karibu 20 ya shule zilizokuwa zikisimamiwa na makanisa ya Katoliki na Protestani kwa ufadhili wa serikali, ambapo watoto walilazimishwa kutengana na familia zao, kupigwa marufuku kuzungumza lugha zao na mara nyingi kunyanyaswa.

"Wengi wa watoto hao walizikwa katika makaburi yasiyo na alama au yaliyotunzwa vibaya huku wakizikwa mbali na Makabila yao ya Kihindi.

Idara hiyo ilipata kwa uchache maeneo 53 ya maziko katika au karibu na shule za bweni. Idadi ya vifo vinavyojulikana, ambavyo vilisababishwa na magonjwa, majeraha ya ajali na unyanyasaji, vinaweza kupanda hadi maelfu au hata makumi ya maelfu, idara hiyo ilisema.

Ripoti hiyo inahusu hadi zaidi ya shule 400 ambazo zilianzishwa au kuungwa mkono na serikali ya Marekani kupitia makanisa kuanzia mwanzoni mwa karne ya 19 na kuendelea katika baadhi ya matukio hadi mwishoni mwa miaka ya 1960.

"Kila mmoja wa watoto hao ni mwanafamilia aliyepotea, mtu ambaye hakuweza kutimiza lengo lake katika dunia hii kwa sababu walipoteza maisha yao kama sehemu ya mfumo huu mbaya," amesema Katibu wa Mambo ya Ndani Deb Haaland, ambaye babu zake walikuwa katika shule ya bweni kwa miaka kadhaa.

Akizungumza katika mkutano wa wanahabari siku ya Jumatano, Haaland alielezea jinsi enzi ya shule ya bweni iliendeleza umaskini, matatizo ya afya ya akili, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vifo vya mapema katika jamii za wakazi asili wa Amerika.

Ripoti hiyo mpya inakuja miezi kadhaa baada ya kugunduliwa kwa mamia ya makaburi ambayo hayana alama katika maeneo ya shule za zamani nchini Kanada ambayo yalileta kumbukumbu chungu kwa jamii za Wenyeji.

Kugunduliwa makaburi ya mamia ya watoto wa Wakanada asili waliokuwa wakishikiliwa kwa lazima katika shule za wamishonari wa Kikatoliki kumezua wimbi kubwa la hasira kati ya raia wengi wa nchi hiyo, taasisi za kutetea haki za binadamu na baina ya wapenda haki kote duniani.

Kugunduliwa kwa mabakuri hayo ya watoto ni ushahidi madhubuti wa ubaguzi wa rangi na wa kimbari uliofanywa dhidi ya wenyeji asili wa Kanada na Marekani.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*