?>

Polisi Msumbiji: Magaidi 37 wenye mfungamano na Daesh wauawa kaskazini mwa nchi hiyo

Polisi Msumbiji: Magaidi 37 wenye mfungamano na Daesh wauawa kaskazini mwa nchi hiyo

Polisi ya Msumbiji imeeleza kuwa jana iifanikiwa kuwaangamiza magaidi 37 katiak oparesheni ya vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kaskazini mwa nchi.


Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Polisi ya Msumbiji imeeleza kuwa, vikosi vya ulinzi vya jeshi la nchi hiyo viliendesha oparesheni katika wilaya ya Macomia kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo na kufanikiwa kuwauwa magaidi 37. 

Wilaya ya Macomia ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa na machafuko huko Msumbiji. Magaidi wenye mfungamano na kundi la kigaidi na kitakfiri a Daesh wapo katika eneo hilo. 

Vikosi vya ulinzi vya  Msumbiji mbali na kuwauwa magaidi hao wa Daesh vimefanikiwa kunasa pia silaha 21. Inspekta jenerali wa polisi ya Msumbiji Bernardino Rafael amesema kuwa, katika oparesheni ya karibuni iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo katika wilaya ya Macomia wakamata magari matatu, pikipiki kumi, baiskeli tisa huku magari ya magaidi zaidi ya 17 yakiharibiwa.  

Jimbo la Cabo Delgado huko kaskazini mwa Msumbiji lilianza kushuhudiwa mashambulizi ya wanamgambo wenye mfungamano na kundi la Daesh mwaka 2017. Mashambulizi hayo yaliongezeka sana mwaka huu na kusababisha kudhibitiwa miji muhimu kwa muda kadhaa sambamba na kushambuliwa maeneo ya kijeshi na yale ya kistratejia. 

 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni