?>

Watu 46 wauawa katika shambulio la kundi la waasi wa ADF mashariki mwa DRC

Watu 46 wauawa katika shambulio la kundi la waasi wa ADF mashariki mwa DRC

Raia wasiopungua 46 wanaripotiwa kuuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya waasi kufanya mashambulio mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Duru za usalama zinaripoti kwamba, jana Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishuhudia moja ya siku ya umwagaji damu mkubwa baada ya kundi la waasi wa ADF kufanya mashambulio mashariki mwa nchi hiyo na kuua kwa akali watu 46 na kujeruhi makumi ya wengine.

Adio Gidi, Waziri wa Mambo ya Ndani huko Ituri amewaambia waandishi wa habarii kwamba, tumepokea taarifa za shambulio la waasi wa ADF na ripoti za karibuni kabisa zinaonyesha kuwa, raia 46 wameuawa katika shambulio hilo.

Maeneo yanayoizunguka Beni, Irumu na Mambasa yamekuwa yakilengwa na mashambulio ya waasi wa ADF kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.

Tarehe 7 mwezi huu watu wasiopungua 22 waliuawa pia katika shambulizi lililofanywa na waasi hao katika mkoa wa Kivu Kaskazini huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kundi la hilo la waasi linalotokea kaskazini mashariki mwa Uganda limekuwa likiendesha shughuli zake katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu muongo wa 90, ambapo limeua mamia ya watu, mbali na kupelekea malaki ya wengine kuwa wakimbizi. 

Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likishuhudia machafuko ya mara kwa mara baina ya makundi ya wanamgambo kwa upande mmoja na wanamgambo na maafisa usalama kwa upande mwingine, kutokana na kuwa na utajiri mkubwa wa madini hususan dhahabu na almasi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni