?>

Watu 81 waaga dunia kwa mafuriko nchini Ujerumani huku makumi wakitoweka

Watu 81 waaga dunia kwa mafuriko nchini Ujerumani huku makumi wakitoweka

Idadi watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika siku mbili zilizopita magharibi mwa Ujerumani imefikia watu 81 leo huku makumi9 ya wengine wakiwa bado hawajulikani walipo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Viongozi wa eneo hilo nchini Ujerumani wameziambira duru za habari kwamba, baadhi ya watu wasiopungua 1,300 bado hawajulikani waliko katika eneo pekee la Ahrweiler, kusini mwa Cologne, katika Kaunti ya Rhineland-Palatinate.

Mtandao wa simu haufanyi kazi tena katika maeneo mengine yaliyoharibiwa na mafuriko, mawasiliano yamekatika kabisa hali ambayo imezikwamisha familia zilizo katika shida kuwasiliana na ndugu zao kwa ajili ya kupatiwa msaada.

Mafuriko hayo makubwa yameharibu kabisa miji na vijiji vingi huko North Rhine-Westphalia na Rhineland-Palatinate tangu usiku wa Jumatano hadi Alkhamisi ya jana.

Mamlaka husika zimetangaza kuwa, baadhi ya nyumba zimeanguka leo Ijumaa asubuhi huko Erftstadt, karibu na Cologne, ambapo juhudi za kutoa misaada kwa wakazi zimekwama kusaidia wakaazi ambao walirudi nyumbani hivi karibuni licha ya onyo.

Mafuriko hayo pia yamesababisha uharibifu mkubwa nchini Ubelgiji, ambapo watu wengi wamehamishwa, hasa katika jiji la Liège.

Bwawa la Rurtalsperre, lililoko upande wa Ujerumani kwenye mpaka na Ubelgiji, liliharibiwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa na lingine liko hatarini, viongozi wamesema.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Horst Seehofer ameliambia Gazeti la Der Spiegel kwamba serikali ya shirikisho itatoa msaada wa kifedha wa dharura kwa maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko. Serikali inatarajiwa kuipitisha msaada huo katika Baraza la Mawaziri Jumatano ya wiki ijayo.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*