?>

Watu wanne wauawa katika shambulio la watu wenye silaha Cameroon

Watu wanne wauawa katika shambulio la watu wenye silaha Cameroon

Wanafunzi watatu na mwalimu mmoja wameuawa katika shambulio la watu wenye silaha wasiojulikana baada ya kuishambulia shule moja katika jimbo lililoathiriwa na machafuko kusini magharibi mwa Cameroon.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Taasisi moja la Kutetea Haki za Binadamu limeeleza kuwa wanafunzi hao waliokuwa na umri wa miaka 12, 16 na 17 pamoja na mwalimu wao wa lugha ya Kifaransa wameuawa katika shambulio ohilo huko Ekondo Titi jimbo lililoathiriwa na machafuko huko kusini magharibi mwa Cameroon.  

Kituo hicho kwa jina la The Centre for Human Rights and Democracy in Africa (CHRDA) kimesema jana katika taarifa yake kuwa wanafunzi wengine kadhaa wameshambuliwa pia katika shambulio hilo huko Ekondo Titi. Kituo hicho cha haki za binadamu kimelaani vikali kitendo cha kushambuliwa wanafunzi na walimu na kuitaka serikali ya Cameroon kuchukua hatua ipasavyo kuchunguza tukio hilo.

Mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka minne sasa katika jimbo linalozungumza lugha ya Kiingereza nchini Cameroon ulianza pale vikosi vya serikali vilipoanza kutumia mabavu kukandamiza maandamano ya amani ya mawakili na walimu wanaopinga kutengwa na serikali kuu inayozungumza lugha ya Kifaransa. Katika kukabiliana na hatua hiyo, makumi ya makundi yenye silaha yaliundwa ili kupigania kuundwa  nchi yao huru kwa jina la Ambazonia. 

Watu wasiopungua 4,000 wameaga dunia hadi sasa katika machafuko huko Cameroon huku wengine zaidi ya laki saba wakilazimika kuhama makazi yao. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*