?>

Watu watano waaga dunia katika mlipuko wa bomu karibu na shule huko Mogadishu

Watu watano waaga dunia katika mlipuko wa bomu karibu na shule huko Mogadishu

Watu watano wameuawa na wengine zaidi ya 12 wamejeruhiwa hii leo katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na shule moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mohamed Abdillahi afisa usalama mjini Mogadishu ameeleza kuwa, hadi sasa wamethibitisha kuaga dunia watu 5 na 15 kujeruhiwa katika mlipuko huo wa bomu. Ameongeza kuwa wanafunzi 11 ni miongoni mwa majeruhi. 

Amesema hawafahamu shambulio hilo lilikusudiwa kina nani kwa kuwa kulikuwa na gari ya ulinzi binafsi iliyokuwa ikisindikizwa katika njia hiyo karibu na mahali pa tukio. Wakati huo huo Abdiladir Abdirahman Mkurugenzi wa Huduma za Ambulance za Aamin huko Mogadishu ameutaja mlipuko huo wa bomu kuwa ni maafa. 

Hakuna kundi lililojitokeza na kukiri kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi hata hivyo wanamgambo wa kundi la Al Shabaab wamedai kuhusika na matukio mengine ya milipuko huko Mogadishu likiwemo shambulio kubwa la mauaji la mapema Jumamosi lililosababisha kifo cha mwandishi habari mtajika wa Somalia Abdiaziz Mohamud Guled. Guled alifahamika kama mkosaji mkubwa wa magaidi wa mtandao wa al Qaida.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*