?>

Watu zaidi ya 30 wapoteza maisha Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi

Watu zaidi ya 30 wapoteza maisha Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi

Watu zaidi ya 30 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Indonesia baada ya kutokea tetemeko la ardhi katika moja ya visiwa vya nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waokoaji nchini Indonesia, wanawatafuta watu kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Sulawesi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.2 kwa kipimo cha richter lilitokea Ijumaa asubuhi, na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa.

Maelfu ya watu wengine, wamebaki bila makazi baada ya tetemeko hilo kusababisha hasara katika kisiwa hicho.

Kisiwa cha Sulawesi kina historia ya kutokea kwa majanga ya tetemo la ardhi na tsunami na mwaka 2018 watu zaidi ya elfu mbili walipoteza maisha baada ya majanga hayo mawili.

Mbali na makaazi ya watu kuporomoka, majengo ya serikali ikiwemo hopsitali, zimeporomoka pia na kusababisha hasara kubwa.

Mwaka 2004, watu 226,000 walipoteza maisha katika kisiwa cha Sumatra baada kutokea kwa tetemeko la ardhi.

Janga hilo la kimaumbile linatokea siku chache tu baada ya ndege ya abiria ya nchi hiyo ambayo iliripotiwa kupoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jakarta, kuthibitishwa kkwamba imeanguka baharini ikiwa na abiria 62 wakiwemo watoto 10.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni