?>

Wayemeni 80,000 wamefariki kwa kukosa matibabu nje ya nchi baada ya uwanja wa ndege wa Sana'a kufungwa

Wayemeni 80,000 wamefariki kwa kukosa matibabu nje ya nchi baada ya uwanja wa ndege wa Sana'a kufungwa

Wizara ya usafiri na uchukuzi ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen imesema, watu 80,000 wamefairki dunia kwa sababu ya kufungwa kwa muda wa miaka sita uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sana'a.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumatatu na wizara hiyo pamoja na idara zilizo chini yake, kutokana na hasara na madhara makubwa yaliyosababishwa na uvamizi wa kijeshi ulioanzishwa na Saudi Arabia, kuwekewa mzingiro Yemen na kufungwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sana'a kwa muda wa miaka sita, raia 80,000 wa nchi hiyo waliokuwa wakihitaji matibabu ya haraka wameaga dunia baada ya kushindikana kuwasafirisha kuwapeleka nje ya nchi.

Wizara ya usafiri na uchukuzi ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen imebainisha katika ripoti yake kuwa, kuna wagonjwa zaidi ya laki nne na nusu ambao wanahitaji kupelekwa haraka nje ya nchi kwa ajili ya kuendelea na matibabu, lakini mzingiro iliowekewa nchi hiyo umewazidishia machungu na maumivu ya maradhi waliyonayo.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo imeeleza kwamba, katika kipindi chote hicho, muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia umeteketeza magari na malori ya mafuta 1,083 na kubomoa barabara na madaraja 4,490 na vyombo 7,229 vya usafiri.

Wizara ya usafiri na uchukuzi ya serikali ya uokovu ya Yemen imebainisha pia kwamba, mgonjwa mmoja kati ya kila wagonjwa kumi wanaolazimika kutumia njia ya barabara ili kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu wakitoka Sana'a kuelekea uwanja wa ndege wa Aden au Seyoun hufariki dunia njiani wakielekea viwanja hivyo vya ndege ambavyo viko kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali kibaraka wa Saudi Arabia.

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro nchi hiyo wa nchi kavu, baharini na angani ambao unaendelea hadi sasa. Moto wa vita uliowashwa na Saudia na washirika wake umeshaua raia zaidi ya 43,000, wakiwemo watoto 7,999 na wanawake 5,184, umejeruhi maelfu na kuwafanya wakimbizi mamilioni ya raia wengine wa Yemen.../  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*