?>

Wazayuni wazidi kuharibu athari za kihistoria za Wapalestina

Wazayuni wazidi kuharibu athari za kihistoria za Wapalestina

Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameanza kuchukua hatua za kuvunja makaburi makubwa zaidi ya watu wa Canaan yaliyoko katika eneo la al Khidhr la kusini mwa Bayt al Lahm.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya al Alam imeripoti habari hiyo na kumnukuu Hassan Brijieh, mkuu wa ofisi ya Kamati ya Kukabiliana na Ujenzi wa Ukuta na Vitongoji vya Walowezi wa Kizayuni akisema hayo leo Ijumaa na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni umelisafisha eneo hilo lililoko baina ya Quds na al Khalil lenye ukubwa wa hekta 4 kwa madai ya kupanua barabara.

Brijieh ameongeza kuwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa kitendo hicho cha utawala wa Kizayuni ni uvunjaji wa wazi wa haki za Wapaletina, ni uvamizi wa mchana kweupe na ni kuangamiza turathi za kale za kihistoria za Wapalestina na vile vile ni jinai ya kivita dhidi ya wananchi na historia ya taifa la Palestina.

Kila leo utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya jinai dhidi ya matukufu ya Wapalestina na Waislamu. Cha kusikitisha ni kuona kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu, kama Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), zinazidi kujikomba kwa Wazayuni na kufungua balozi zao katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Kuvuruga utambulisho wa Kiislamu wa Palestina kama kuvunja maeneo ya kihistoria ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, ni katika siasa kuu za Israel na hili ni suala ambalo kila Muislamu na kila mpenda haki anapaswa kusimama imara kulikemea kwa kadiri anavyoweza.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*