?>

Waziri Mkuu wa zamani wa Algeria ahukumiwa kifungo miaka 7 jela

Waziri Mkuu wa zamani wa Algeria ahukumiwa kifungo miaka 7 jela

Mahakama nchini Algeria imemhukumu kifungo cha miaka 7 jela Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo kwa kufanya ufisadi katika sekta ya utalii katika mkoa wa Skikda kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mahakama Maalumu ya Kupambana na Ufisadi wa Fedha na wa Kiuchumi katika manispaa ya Sidi M'Hamed katika mji mkuu, Algiers jana Jumatatu ilitoa hukumu kwa waliohusika na ufisadi katika sekta ya utalii katika mkoa wa Skikda na hivyo kumhukumu kifungo cha miaka saba jela Ahmed Ouyahia, Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo na faini ya kulipa dinari milioni moja sawa na zaidi ya dola za Kimarekani 7,500.   

Mahakama hiyo ya Algeria pia imewahukumu watuhumiwa wengine wa kesi hiyo ya ufisadi katika sekta ya utalii mkoani Skikda yaani Ammar Ghoul na Abdulghani Zaalan mawaziri wa zamani wa usafirishaji na shughuli za umma wa nchi hiyo kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya dinari milioni moja.  

Kwa mujibu wa hukumu hio ilizotolewa na mahakama Maalumu ya Kupambana na Ufisadi wa Fedha na wa Kiuchumi ya Algeria, Mohamed Bouderbali Gavana wa zamani wa mkoa wa Skikda naye amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kulipa faini ya dinari milioni moja. Magavana wengine wawili wa zamani wa mkoa huo pia wamekuhukumiwa kwenda jela miaka miwili na kulipa faini kwa kuhusika kwao katika kesi ya ufisadi.  

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni