?>

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan aitisha maandamano ya amani dhidi ya serikali

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan aitisha maandamano ya amani dhidi ya serikali

Imran Khan Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan ametangaza kuitisha maandamano ya amani dhidi ya serikali ya Islamabad.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Imran Khan ambaye aliondolewa madarakani hivi karibuni na Bunge la Pakistan amesema kuwa, ataongoza maandamano ya amani dhidi ya serikali kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Islamabad wiki hii kwa shabaha ya kushinikiza madai yake ya kuitishwa uchaguzi mpya.

Imran Khan amewataka wafuasi wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) na wananchi wa Pakistan kwa ujumla kufika mjini Islmabad ili kujiunga na mkutano wake unaoanza kesho Jumatano akisema kuwa, mkutano huo hatimaye utageuka kuwa maandamano ya kupinga na kuendelea kushinikiza matakwa yake yatekelezwe.

Imran Khan bingwa wa zamani wa mchezo wa kriketi, alivuliwa wadhifa wa Uwaziri Mkuu na Bunge la Pakistan mwezi uliopita wa Aprili baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kupelekea kuundwa serikali mpya nchini humo.

Imran Khan amekuwa akisisitiza kuwa, anataka ufanyike uchaguzi wa mapema na kuonya kuwa endapo serikali iliyopo haitatekeleza takwa lake hilo ataitisha maandamano ya mamilioni ya watu kuelekea mji mkuu Islamabad.

Hivi karibuni Imran Khan alidai kuwa, njama za kutishia maisha yake zinaendelea kufanywa ndani na nje ya nchi hiyo na kwamba amesharekodi mkanda wa video wenye majina ya watu wote wanaokula njama dhidi yake.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*