?>

Waziri wa Habari wa Sudan: Kufanya mapatano na Israel hakutaleta amani na utulivu

Waziri wa Habari wa Sudan: Kufanya mapatano na Israel hakutaleta amani na utulivu

Waziri wa Habari wa Sudan amesema, ahadi ya kupata amani na utulivu nchi zilizofanya mapatano na utawala wa Kizayuni ni njozi tupu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Faisal Muhammad Saleh ameeleza kwamba, yaliyozungumzwa kuhusu kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kwamba sera hiyo itaziletea amani na utulivu pande zilizofanya mapatano hayo ni njozi na dhana tupu.

Muhammad Saleh ameongeza kuwa, watu wengi nchini Sudan walioafiki suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni walifanya hivyo kwa ajili ya kuondolewa vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo na Marekani.

Mnamo mwanzoni mwa mwaka huu wa 2020 Benki Kuu ya Sudan ilitangaza kuwa, Marekani imekusudia kuiondolea vikwazo vyote vya kiuchumi nchi hiyo isipokuwa vile vichache tu vinavyohusiana na kadhia ya Darfur.

Baadaye mnamo mwezi Septemba, rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa amekusudia kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Hatimaye, na baada ya kupita miaka 27 ya vikwazo, uamuzi huo wa serikali ya Trump ulitekelezwa na Bunge la nchi hiyo ndani ya kipindi cha siku 45.

Uamuzi wa serikali ya mpito ya Sudan wa kukubali kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umewaghadhibisha wananchi wengi wa Sudan. 

Mbali na upinzani wa wananchi, Baraza la Fiqhi ya Kiislamu la nchi hiyo pia limetoa taarifa likisisitiza kwamba, ni haramu kuanzisha uhusiano wowote na utawala huo ghasibu unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina..

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni