?>

Waziri wa Ulinzi asisitiza kuongezwa uwezo wa jeshi la majini la Iran kulingana na ukubwa wa vitisho

Waziri wa Ulinzi asisitiza kuongezwa uwezo wa jeshi la majini la Iran kulingana na ukubwa wa vitisho

Akiwa ziarani katika mkoa wa Hormozgan kusini mwa Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametembelea miradi ya majini ya wizara hiyo huko Bandar Abbas hususan utengenezaji wa manowari, meli za kawaida za kivita na nyambizi na kusema kuwa kuimarishwa nguvu katika pande zote za ulinzi ikiwa ni pamoja na nchi kavu anga, na hasa baharini, ni moja ya vipaumbele vya mipango ya ulinzi wa nchi.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Brigedia Jenerali Ashtiani amesema eneo la kijiografia la Iran na hasa katika maji ya Ghuba ya Uajemi lina umuhimu wa kistratijia, na kuongeza kuwa: Wizara ya Ulinzi itaimarisha nguvu na kulipa jeshi vifaa na zana zinazohitahika ili kukidhi mahitaji yake na kuliwezesha kukabiliana na vitisho vya kikanda katika maji yake yote.

Jeshi la Wanamaji linazingatiwa na kuchukuliwa kimataifa kuwa chombo muhimu kwa ajili ya kulinda usalama wa majini na maslahi ya mataifa mbalimbali na hata nje ya mipaka ya mataifa hayo na kwa hivyo ni jeshi linalohitaji kudhaminiwa zana zanazofaa na za kisasa kwa ajili ya kutekeleza vyema majukumu yake. Umuhimu wa Jeshi la Wanamaji kwa  ajili ya kulinda usalama wa kitaifa na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni nchi yenye pwani ndefu kwenye mpaka wake wa kaskazini na kusini, na kwa upande mwingine ikiwa kwenye eneo nyeti na lililo na umuhimu mkubwa wa kistratejia la Ghuba ya Uajemi, ni jambo lisilopingika.

Kwa kuzingatia hilo na kwa kutilia maanani ukweli kwamba Iran imekuwa chini ya vikwazo vya silaha kwa miongo kadhaa, ni jambo la dharura kwa Iran kuzingatia uwezo wake wa ndani katika kujidhaminia zana za ulinzi wa baharini na zana za kijeshi kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC. Majeshi hayo yakiwa ni nguzo mbili muhimu ya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kila moja likiwa na majukumu maalumu ya kudhamini usalama wa maji ya Iran na pia nje ya mipaka ya nchi, yanahitaji kuwa na silaha za kutosha zilizotengenezwa ndani ya nchi kwa ajili ya kuyawezesha kutekeleza vizuri majukumu yao.

Katika miaka ya hivi karibuni na kutokana na umuhimu wa kuimarisha nguvu na silaha za majini pamoja na umuhimu wa kuwepo kwa ufanisi katika maji ya kitaifa na kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewekeza pakubwa katika uwanja wa kudhamini silaha mbali mbali za majini. Kwa kadiri kwamba hii leo imefanikiwa kujitengenezea vifaa na zana mbalimbali za ulinzi wa baharini, manowari, nyambizi na mifumo tofauti ya hujuma baharini na kuzikabidhi kwa majeshi yake ya kawaida na ya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC au kwa jina jingine, Sepah.

Vifaa na zana hizi zilizotengenezwa ndani ya nchi na wataalamu wa Kiirani, ikiwa ni pamoja na vyombo vyepesi na vizito, manowari, boti za mwendo kasi, aina mbalimbali za makombora ya kushambulia meli na vifaa vingine kama vile ndege zisizo na rubani zilizowekwa kwenye manowari pamoja na aina tofauti za boti za hujuma, sio tu kwamba zimeongeza uwezo wa kiulinzi wa Jeshi la Wanamaji la Iran, bali pia linatuma ujumbe mzito kwa nchi za kikanda na kimataifa kuhusu utayarifu kamili wa Iran katika kukabiliana na tishio lolote na uvamizi katika maji yake.

Hata hivyo, kama inavyosisitiza mara kwa mara, Iran inataka amani na utulivu katika maji yake yote hasa katika Ghuba ya Uajemi, na kwa hivyo uwepo katika eneo wa nchi ajinabi na chokozi hususan Marekani unahesabiwa kuwa sababu ya ukosefu wa utulivu na usalama katika eneo hili nyeti na la kistratijia.

Kuhusiana na suala hilo, Brigedia Jenerali Ashtiani amesema: Ujumbe wa Iran kwa eneo na dunia nzima ni ujumbe wa amani na utulivu, na katika upande mwingine tunaamini kuwa amani na utulivu wa eneo unaweza kupatikana kwa kuwepo na kushirikishwa mataifa yote ya eneo katika kudhamini usalama. Iran inaamini kuwa uwepo wa wageni na majeshi ya kimataifa ndicho chanzo cha ukosefu wa usalama katika eneo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kusita na wala haitasita hata kidogo katika kutetea maslahi yake ya kitaifa na kuondoa vitisho.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*